Episodes

9 hours ago
9 hours ago
MBEGU ZA WATU
Watu ni mbegu. Ni aina gani ya watu wamepandwa kwenye Maisha yako. Aina ya watu waliokuzunguka itaamua aina ya mavuno kwenye Maisha yako
Baadhi ya watu ni magugu na wengine ni Mbegu Njema
Wewe mtoto wa Ufalme ni Mbegu Njema. JIfunze Zaidi kwenye somo hili namna unavyoweza kuzaa sana kuwa baraka kwenye ulimwengu wako:

7 days ago
7 days ago
NGUVU YA MANENO
Maneno unayoyaongea ni Muhimu kuliko chochote kwenye Maisha yako
Maisha yako yamejaa matunda ya midomo yako.
Jifunze Zaidi kwenye somo hili:

Thursday Apr 24, 2025
Thursday Apr 24, 2025
NGUVU YA FIKRA
Fikra zako ni Muhimu kuliko Fikra za Mungu.
Fikra za Mungu zinakua na tija pale zinapofanyika kuwa fikra zako.
Fikra za Mungu juu ya Israel ilikua ni kuwapeleka kwenye nchi inayotiririka maziwa na asali lakini baadhi yao walijaa fikra za matango, matikiti na vitunguu swaumu vya Misri hivyo hawakuweza kuingia nchi ya Ahadi.
Fikra zao zilikinzana na Fikra za Mungu hivyo hawakuweza kufurahia mema aliyowawazia.
Fikra ni Mbegu, na Maisha yako ni Mavuno ya mbegu za fikra zilizopandwa kwenye moyo wako.
Jifunze Zaidi kwenye somo hili litalobadilisha Maisha yako milele

Thursday Apr 24, 2025
Thursday Apr 24, 2025
FAITH FOR WARFARE
Maisha yana vita na kukataa uwepo wa vita hakuondoi vitaKitachokupa faida ni kuwa tayari kwa ajili ya vita kwa Kuvaa silaha zoto za Mungu (Efeso 6:11)
Adui hana nguvu ila alichonacho ni HILA (Efeso 6:11). Msingi wa Hila ni Uongo na Msingi wa Imani ni KWELI YA NENO LA MUNGU.
Ngao ya Imani ndio silaha pekee ya kukukinga na mishale ya moto ya adui
Ufanisi wa Ngao yako unatemea kiwango cha kweli kilichoko ndani yako (Yohana 8:32)
Mungu amekuambia nini kuhusu Afya Yako, Uchumi, Familia, Watoto, n.k
Maarifa ya neno uliyonanyo kuhusu maeneo mbalimbali ya Maisha yako ndio yatayokupa ulizi pale vita itapoinuka kwenye eneo lolote kweye Maisha yako kwakua unajua vita inatokana na HIla (Uongo) na Imani yako ni Imara kwakua Imejengwa Juu ya Kweli ambayo ni Neno Na Mungu.
Jifunze Zaidi kwenye somo hili:

Friday Apr 11, 2025
Friday Apr 11, 2025
KANUNI YA MBEGU - MAWAZO
Unachowaza kuhusu wewe na maisha yako ni Muhimu kuliko kile Mungu au shetani anawaza kuhusu wewe.
Mawazo yako yanaweza leta mauti au uzima kwenye maisha yako.
Jifunze Zaidi kwenye somo hili:

Monday Apr 07, 2025
Monday Apr 07, 2025
Namna unvyopokea neno inaamua matokeo ya maisha yako.
Kwa wana wa Mungu hatupokea neno la Mungu passively (dichomai) bali TUNALICHUKUA (Lambano)
Wengi wamekaa passively wakisubiri Bwana atende wakati Bwana ameshawapa kila kitu kifaacho kwa ajili ya uzima na utaua (2 Petro 1:3). Kinatochakiwa ni wao KUCHUKUA kile kilichoko ndani yako katika Kristo.
Mat 21:22 Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea (Lambano).
Neno mtapokea ni neno la Kiyunani LAMBANO likiimanisha kuchukua kwa ujasiri kama mtu anayechukua kile kilicho chake.
Mwana wa Mungu chukua maisha ya utukufu uliyoitiwa kuishi
Jifunze Zaidi kwenye somo hili

Friday Apr 04, 2025
Friday Apr 04, 2025
KANUNI YA MCHAKATO - PT 2
Kwenye sehemu ya pili ya somo hili tunaangalia faida ya mchakato.
Mungu huwapa watu sawasawa na uwezo wao: Mathayo 25:15“Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja, kila mtu kadiri ya uwezo wake; akasafiri mara.
Ili kufanya makubwa Zaidi badala ya kukaa na wishful thinking chukua hatua na kuongoza capacity (uwezo wako). Hatima ni kwa wanaoweza kupambana (fighters) na wanaoweza kutamalaki territories.
Kutembea katika halisia za baraka tulizo nazo katika Kristo ni Zaidi ya kufunga, kuomba na kusoma neno.
Jifunze Zaidi kwenye somo hili:

Thursday Apr 03, 2025
Thursday Apr 03, 2025
IWENI WATENDAJI WA NENOYak 1:22-25 Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Maana mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, huyo ni kama mtu anayejitazama uso wake wa asili katika kioo; Lakini yeye anayeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.1. Ni udanganyifu kuwa msikiaji wa Neno pekeeMt 7:24-27 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile; nayo haikuanguka, kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga, mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba hiyo; ikaanguka: na anguko lake lilikuwa kubwa. 2. Anguko katika maisha si kwa sababu ya yale tunayokabiliana nayo bali ni yale tunayofanyaJifunze zaidi kwenye somo hili

Thursday Mar 27, 2025
Thursday Mar 27, 2025
KANUNI YA MCHAKATO
Kila mafanikio ya kweli na ya kudumu yanahitaji mchakato. Kwenye kanuni ya mbegu kumea kuna mchakato.Mark 4:28Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke.Wengi wanakata tamaa wanapokutana na ugumu au changamoto kwenye maisha hasa wanapoona Njozi au kusudi la maisha yao inachelewa. Hii inatokana na kutokuelewa KANUNI YA MCHAKATO.
Mafanikio yako ni UHAKIKA. Kaa kwenye Mchakato.If you jump up you will come done but if you grow up you will stay there.
Ukuaji wa ghafla sio ukuaji ni uvimbe😂
Jifunze Zaidi kwenye Somo Hili

Thursday Mar 27, 2025